Katika miaka ya hivi karibuni kumeibuka habari kuhusu ukatili unaofanywa dhidi ya watoto. Hii siyo tena jambo la ajabu.
Baadhi ya ukatili huo ni pamoja na kubakwa na ule wa kukatwa viungo vya mwili kwa watoto wenye ulemavu wa ngozi (albino).
Licha ya kupigiwa kelele, hata kampeni mbalimbali
za kupinga kufanyika, unyama huo umeendelea kufanyika na tukio la hivi
karibuni limemhusisha mtoto Erisia Tito mwenye miezi miwili anayedaiwa
kunajisiwa wilayani Mpwapwa Mkoa wa Dodoma.
Tukio hilo limekuwa gumzo katika mitaa mbalimbali
wilayani humo, huku baadhi ya wananchi wakidai kuwa linahusiana na imani
za kishirikina.
Unaweza kujiuliza maswali mengi, hata inakuwaje mtoto wa miezi miwili kunajisiwa?
Katika
vijiwe vya kahawa wilayani Mpwapwa, hii ni habari kubwa zilizokuwa
zikizungumzwa kuhusu kunajisiwa kwa mtoto huyo swali likibaki; Je,
yule mtu alimnajisi mtoto ameishia wapi?
Naingia chumba cha Mganga Mkuu Wilaya ya Mpwapwa
kupata maelezo ya mtoto huyo tangu alipofikishwa katika hospitali ya
wilaya hiyo, maendeleo yaliyofikiwa na utaratibu wa kiuchunguzi
unavyoendelea.
Kauli ya Mganga Mkuu
Mganga
Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Mpwapwa, Lunemo Sakafu anasema kuwa tangu
alipolazwa, mtoto huyo alikuwa akipelekwa kliniki kwa ajili ya kupatiwa
chanzo mbalimbali na kupima afya yake, kwamba alikuwa na afya nzuri.
“Hakuzaliwa katika hospitali hii ila alikuwa
akihudhuria kliniki, alizaliwa kwa wakunga wa jadi na mara ya mwisho
kuja hapa hospitali ilikuwa Aprili 15, mwaka huu na alikuwa na afya
nzuri,” alisema
Ashangazwa
Alisema kuwa
alishangazwa na hali aliyokuwa nayo mtoto huyo alipofikishwa kwa mara
nyingine katika hospitali hiyo kwani alikuwa akitokwa haja zote bila
kikomo.
“Tunampatia matibabu ya kina ili kujua tatizo ni
nini. Kwa sasa tuna utaratibu wa kumpeleka katika Hospitali ya Rufaa ya
Dodoma ili akafanyiwe vipimo vya kina kwa kuwa mtoto huyu anatoa haja
zote bila kikomo,” anasema Sakafu.
Sakafu anasema hata wazazi wa mtoto huyo
walipoulizwa juu ya hali aliyonayo mtoto wao, walipishana kauli katika
maelezo yao na kwamba jambo hilo liliwatia shaka.
No comments:
Post a Comment