Pages

Thursday, May 9, 2013

Mbaroni kwa kukutwa na vifaa vya noti bandia

JESHI la Polisi Mkoa wa Katavi limemkamata Hilali Abdalah (30), mkazi wa Mtaa wa Majengo kwa tuhuma za kukutwa na vifaa vya kutengenezea noti bandia.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi, Dhahiri Kidavashari, alisema Hilali alikamatwa juzi, majira ya ssa 8 mchana katika nyumba ya kulala wageni inayoitwa Ambassador iliyoko Mtaa wa Mji wa Zamani, Kata ya Kashaulili, mjini hapa.

Alisema mtuhumiwa alikamatwa kutokana na taarifa za kiintelejensia kulifikia Jeshi la Polisi mkoani Katavi kutoka kwa raia wema.

Alivitaja vifaa alivyokamatwa navyo mtuhumiwa kuwa ni karatasi ngumu 217 ambazo hutumika kutengenezea noti bandia za sh 10,000, bomba mbili za sindano zenye dawa maalumu kwa ajili ya kubadilishia rangi ya karatasi hizo, ili zifanane na pesa hizo.

Vifaa vingine ni poda chupa moja, beseni moja kwa ajili ya kusafishia karatasi hizo mara baada ya kuzipitishia kwenye hatua kadhaaAlisema awali mtuhumiwa alikuwa akijihusisha na uuzaji wa mitumba katika Soko la Buzogwe mjini hapa na baadaye kuhamia mkoani Tanga ambako alipata ujuzi wa kutengeneza noti bandia na kisha kurejea Mpanda.

No comments:

Post a Comment